HALMASHAURI YA WILAYA YA TANDAHIMBA
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA ROBO YA KWANZA (JULAI- SEPTEMBA) KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023.
Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya Tandahimba iliidhinishiwa kukusanya,kupokea na kutumia jumla ya shilingi 9,483,673,050.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 1,344,250,000 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu,Shilingi 6,837,599,010 ni fedha za ruzuku kutoka kwa Wafadhili na Shilingi 1,301,824,040 ni fedha kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hali halisi ya mapato na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo kwa bajeti ya mwaka 2022/2023 hadi kufikia Septemba 30,2022 (Robo ya kwanza), Halmashauri ilikuwa imepokea jumla ya Ths. 270,405,250. kutoka katika vyanzo mbalimbali na kutumia Shilingi.26,425,250 kama inavyoonekana katika Jedwali Na.1 Hapo chini. Matumizi ya fedha zilizopokelewa ni kidogo kwa sababu fedha zimepokelewa mwishoni mwa mwezi Septemba, 2022
Jedwali Na 1: Hali halisi ya Mapato na Matumizi kwa fedha za miradi ya maendeleo kwa robo ya kwanza Julai-Septemba, 2022/2023
NA.
|
JINA LA MRADI
|
FEDHA IDHINISHWA
|
FEDHA TOLEWA
|
FEDHA TUMIKA
|
FEDHA BAKI
|
MAELEZO
|
1.
|
Mradi wa kuchochea maendeleo ya Jimbo (CDCF)
|
75,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
2.
|
Ukamilishaji wa zahanati 2
|
50,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
3.
|
Ununuzi wa vifaa tiba kwa vituo vya Afya na Zahanati
|
650,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
4
|
Ujenzi wa matundu ya vyoo 30 katika shule shikizi za msingi
|
33,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
5
|
Ujenzi wa madarasa 9 katika shule za msingi kongwe
|
180,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
6
|
Ukamilishaji wa maboma 13 shule za msingi
|
156,250,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
7.
|
Ujenzi wa nyumba za Walimu 8 shule za msingi
|
200,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
8
|
Uboreshaji wa miundombinu ya ujifunzaji na ufundishaji kwa shule za msingi ( Boost)
|
1,290,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
9
|
Ujenzi wa miundo mbinu ya choo na mfumo wa maji katika shule za msingi (SWASH)
|
310,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
10.
|
Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Mahuta na ujenzi wa nyumba 2 za walimu 2 in 1 Litehu sekondari (SEQUIP)
|
573,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
11
|
Ukamilishaji wa bweni katika shule ya sekondari Kitama
|
20,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
12
|
Ujenzi wa miundo mbinu ya choo mfumo wa maji na ukarabati wa wodi katika zahanati (WASH)
|
334,000,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
13
|
Miradi ya afya fedha za wafadhili
|
608.049,000
|
70,405,250
|
26,425,250
|
43,980,000
|
Fedha hazijapokelewa
|
14
|
Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)
|
3,702,550,000
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
15
|
Miradi ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri
|
1,301,824,040
|
0
|
0
|
0
|
Fedha hazijapokelewa
|
16.
|
Ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 kwa shule za sekondari 3
|
200,000,000
|
200,000,000
|
0
|
200,000,000
|
Ujenzi upo hatua ya maandalizi
|
JUMLA KUU
|
9,483,673,050
|
270,405,250
|
26,425,250
|
243,980,000
|
Fedha hazijapokelewa
|
Mchanganuo wa hali halisi ya miradi inayotekelezwa kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 umeambatanishwa na taarifa hii. Aidha kwa kipindi hiki pia Halmashauri iliendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya mwaka 2021/2022.taarifa ya miradi hiyo imeambatanishwa pamoja na taarifa hii..
Charles J. Mihayo
Kny: Mkurugenzi Mtendaji (W)
TANDAHIMBA
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa