Education Services
ELIMU YA AWALI NA MSINGI
Kwa upande wa elimu ya msingi, Wilaya ina jumla ya shule 127. Shule zina jumla ya wanafunzi 62058 . Kati ya hawa wavulana ni 30619 na wasichana ni 31439. Aidha idadi ya Wanafunzi wa Awali jumla ni 7906,Wavulana 4023 naWasichana 3883 na vituo vya walimu 5 ambavyo niTandahimba,Mchichira,Mihambwe,Chikongola na Luagala.Jumla ya mahitaji ya WalimuKatika Halmashauri yetu ni 1856 kwa sasa kuna jumla ya Walimu 965 ambapoWanaume 666 na Wanawake 299 kuna upungufu wa Walimu 894.Waratibu kata wapo 32 ambapo Wanaume 26 na Wanawake 6
Uandikishaji katika shule za Awali na msingi kwa mwaka 2022 nikama ifuatavyo:-
Darasa la Awali Jumla ya wanafunzi 7906 sawa na asilimia 98 waliandikishwaambapo Wavulana 4023 na Wasichana 3883
Darasa la kwanza Jumla ya Wanafunzi 7428 sawa na asilimia109 waliandikishwa ambapo Wavulana 3717 na Wasichana 3711
Hali ya Ufaulu ya Darasa la saba katika Halmashauri ya Tandahimbakwa mwaka 2021 waliofanya Mtihaniwa darasa la saba Jumlani 6373,Wavulana 3073 na Wasichana 3300 waliofaulu 4760 sawana asilimia 75
Hali ya Ufaulu wa upimaji wa Kitaifa wa Darasa la nne mwaka 2021,Waliofanya Mtihani 7061 waliofaulu 6655 sawa naasilimia 94.3
Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (EWW&ENMRA)
Wilaya yetu imekuwa na mipango madhubuti ya kumpatia mtu mzimaelimu kupitia programu mbalimbali za Elimu ya watu Wazima kama ifuatavyo:Mpango wa Elimu Kwa Walioikosa (MEMKWA), tuna madarasa ya wanafunzi wa MEMKWA katik shule za msingi za Matogoro, Jangwani, Mnyawa, Tandahimba, Ruvuma,Chikongola, na Mitondi A. Kisomo chenye manufaa (KCM) tuna madarasakwenye vijiji vya Lienje, Pemba, Majengo, Namdowola, Mitondi A na Mitondi B, naMpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) na Kisomo ChaKujiendeleza (KCK). Changamoto zinazoikabili wilaya katika utoaji wa elimu nipamoja na mwamko mdogo wa kieliemu katika jamii, upungufu wa madarasa ya elimuya watu wazima, walimu wenye sifa, upungufu wa nyumba za walimu, ofisi na vifaavya kufundishia na utoro. Baadhi ya malengo katika kipindi hiki cha mpango nipamoja na kuongeza idadi hiyo ya madarasa katika kila shule ya msingi, kuongezaidadi ya watoto, vijana na watu wazima wanaosajiliwa kuhudhuria masomo namafunzo kwenda shule kutoka 80% hadi 95% ya wanaoandikishwa, kupunguza utoroshuleni, kuongeza idadi ya madarasa yanayojengwa, nyumba za walimu, ukarabatiwa majengo, ujenzi wa matundu ya vyoo na kuboresha Kituo cha Ufundi StadiMatogoro ili kiweze kusajili vijana wengi zaidi.
Historia ya Elimu ya Watu Wazima inaanziawakati wa ukoloni, miaka ya mwanzo baada ya uhuru, mara baada ya kutangazwa kwaazimio la Arusha linalohusu siasa ya ujamaa na kujitegemea, wakati wautekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kurekebisha Uchumi (Tanzania EconomicStructural Adjustment Programme) na wakati wa maandalizi na utekelezaji waMpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu (Education Sector Development Programme).Sababu za kuanzisha na kuendeleza mipango ya Elimu ya Watu Wazima zinatokana nanyakati na malengo yake.
Tafsiri ya Elimu ya Watu Wazima (EWW) na ile ya Elimu Nje ya MfumoRasmi (ENMR) zinatofautiana. Hizi ni sekta ndogo mbili kati ya tatu zilizomokwenye mfumo wa elimu ambazo zote lengo lake kuu ni kutoa maarifa, ujuzi nakujenga muelekeo katika haiba na mwenendo wa mtu au jamii.
Elimu ya watu wazima hujumuisha maarifa na ujuzi ambao hutolewakwa watu wazima ili kuinua ubora wa maisha yao kutokana na shughuli au kaziwanazofanya katika mazingira yao. EWW hujumuisha mafunzo ya stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu (KISOMO chenye manufaa na KISOMO cha kujiendeleza) aumasomo ya kujiendeleza katika maswala ya kilimo, ufugaji, afya malezi ya watoto,mazingira, ufundi, uchimbaji madini, uvuvi na maarifa mengineyo na ujuzitofauti tofauti. Mafunzo ya mtaala mpya katika KISOMO cha kujiendeleza (mafunzoya kilimo na mifugo, sayansi kimu, afya na lishe na ufundi) ni sehemu ya EWW.Aidha, kuna mafunzo mengine kwa watu wazima ya taaluma; mfano mafunzo ya cheti(Astashahada), Stashahada (Diploma) na Shahada, yanayotolewa na taasisimbalimbali kama vile Elimu ya Watu Wazima na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ni maarifa na ujuzi unaotolewa bila kujali rika la washiriki na hutolewa Nje ya Mfumo Rasmi wa shule (watoto,vijana na watu wazima). Mfumo huu haufuati muundo wa madarasa kama vile elimuya awali miaka miwili, elimu ya msingi miaka saba, elimu ya sekondari miaka 4.'A' level miaka 2, chuo kikuu miaka 3-6. Hivyo ENMR ni nyumbufu katika muundo(Structure), mitaala (curriculum), walimu, vifaa vya kufundisha (Teachingmaterials), muda wa kusoma (flexible time), na tathmini (Assessment). Mifano yaENMR ni pamoja na Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA), Mpango WaElimu ya Sekondari kwa Walioikosa (MESKWA), Elimu Masafa na Ana kwa Ana (openand distance Learning). Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Chuo Kikuu Huria –Tanzania ni mifano ya taasisi zinazotoa elimu nje ya mfumo rasmi. Kwa ufupi EWWna ENMR ni mifumo ya Elimu ambayo inasisitiza kuwa Elimu haina mwisho au kuishini kujifunza (lifelong learning). Mifumo hiyo inaimarisha mchakato wa kupatamaarifa, ujuzi kazi ambao unasaidia ubunifu na kupata mwelekeo ulio sahihikatika maisha ya mtu.
ELIMU YA SEKONDARI
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ina shule za sekondari 28 ambazo zinajumla ya wanafunzi 11,242 wakiwemo wavulana 5,228 na wasichana 6,014. Shule ya sekondari Tandahimba ina wanafunzi 190 wavulana wanaosoma kidato cha tano na sita (A-level). Pia, shule za sekondari za Halmashauri ya Tandahimba ina walimu 408 wanafundisha masomo ya sayansi, sanaa na biashara.
1.2 Hali ya miundombinu
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inafanya juhudi kubwa katika kujenga na kukarabati miundombinu katika shule za sekondari. Hali ya miundombinu kwa sasa ipo kama ifuatavyo;
Jedwali 1: Hali ya miundombinu
Na |
Aina ya Miundombinu |
Mahitaji |
Yaliyopo |
Upungufu |
1 |
Madarasa
|
334 |
388 |
0 |
2 |
Maabara
|
54 |
53 |
1 |
3 |
Nyumba za walimu
|
439 |
111 |
328 |
4 |
Matundu ya vyoo vya wavulana
|
214 |
147 |
67 |
5 |
Matundu ya vyoo vya wasichana
|
312 |
150 |
162 |
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba yenye shule 28 na wanafunzi 11,242 wa kidato cha kwanza hadi sita inauhitaji wa walimu 489 wakiwemo walimu 67 wa masomo ya sayansi, walimu watatu (3) wa masomo ya biashara, walimu 338 wa sanaa kama inavyoonekana katika jedwali 1.3
Jedwali 2: Mahitaji ya Walimu
|
Mahitaji |
Waliopo |
Upungufu |
Walimu wa Sayansi
|
211 |
67 |
144 |
Walimu wa Biashara
|
14 |
3 |
11 |
Walimu wa Sanaa
|
264 |
338 |
0 |
Jumla kuu
|
489 |
408 |
155 |
1.4 Maendeleo ya Elimu Sekondari
1.4.1 Ujenzi wa shule mpya
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inaendelea kutekeleza Sera ya Elimu na Ufundi 2014 kwa kufanya upanuzi wa fursa za elimu kwa kujenga shule za sekondari mpya tatu kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 . Shule hizo zinajengwa katika Kata za Litehu, Kwanyama, na Mndumbwe. Ujenzi wa shule za sekondari Mndumbwe na Kwanyama umetekelezwa kwa nguvu za wananchi na Halmashauri na shule ya Litehu imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Programme). Katika mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetoa fedha 120,000,000 kati ya Tsh. 200,000,000 kutekeleza ujenzi wa madara matatu(3) katika shule ya mpya ya sekondari Kwanyama na madarasa matatu (3) katika shule mpya ya sekondari ya Mndumbwe.
Jedwali 3: Ujenzi wa shule mpya
Jina la shule
|
Idadi ya madarasa |
Idadi ya wanafunzi (Nafasi zilizopo) |
Hatua iliyofikiwa |
Mndumbwe
|
9 |
80 |
Kazi ya ukamilishaji unaendelea
|
Kwanyama
|
7 |
80 |
Kazi ya ukamilishaji unaendelea
|
Litehu
|
14 |
80 |
Kazi ya ukamilishaji unaendelea
|
1.4.2 Utekelezaji wa ujenzi wa madarasa
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa madarasa kumi (10) kwa gharama ya Tsh. 200,000,000/= kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023. Madarasa haya yanajengwa katika sekondari za Tandahimba (madarasa 4), sekondari ya Kwanyama (madarasa 3) na sekondari ya Mndumbwe (Madarasa 3) madarasa yote yapo katika hatua ya ukamilishaji.
1.4.3 Mfuko wa elimu
Kupitia Mfuko wa Elimu idara ya elimu imepata fedha kiasi cha shilingi 132,600,000/= ambazo zitatumika kutekeleza miradi ya ujenzi katika shule saba za sekondari kama ifuatavyo,
Jedwali 4: Miradi iliyotekelezwa kupitia mfuko wa elimu
NA |
JINA LA SHULE YA SEKONDARI |
FEDHA TOLEWA |
MRADI |
HATUA ZILIZOFIKIWA |
1 |
Mchichira
|
10,000,000
|
Ukarabati wa vyumba viwili (2) vya madarasa
|
Maandalizi ya ujenzi
|
2 |
Chaume
|
6,300,000
|
Ukarabati wa vyumba viwili (2) vya madarasa
|
Maandalizi ya ujenzi
|
3 |
Mkwiti
|
6,300,000
|
Ukarabati wa vyumba viwili (2) vya madarasa
|
Maandalizi ya ujenzi
|
4 |
Kitama
|
59,000,000
|
Ukamilishaji wa bweni la wasichana
|
Maandalizi ya ujenzi
|
5 |
Kitama
|
5,000,000
|
Kutengeneza meza na viti
|
Maandalizi ya ujenzi
|
6 |
Kitama
|
16,000,000
|
Kukarabati hosteli
|
Maandalizi ya ujenzi
|
7 |
Mnyawa
|
30,000,000
|
Ujenzi wa nyumba ya walimu
|
Maandalizi ya ujenzi
|
JUMLA |
132,600,000
|
|
|
Jedwali: 1.4.2.1 MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE TOKA 2019 HADI 2021
MWAKA |
WALIOSAJILIWA |
WALIOFANYA |
DARAJA I |
DARAJA II
|
DARAJA III |
DARAJA IV |
DARAJA 0 |
||||||||||||||
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
|
2019 |
738 |
940 |
1678 |
727 |
917 |
1644 |
63 |
5 |
68 |
101 |
37 |
138 |
199 |
120 |
319 |
475 |
989 |
1464 |
66 |
230 |
296 |
2020 |
669 |
871 |
1540 |
660 |
828 |
1488 |
67 |
13 |
80 |
106 |
44 |
150 |
194 |
152 |
346 |
535 |
1067 |
1612 |
67 |
168 |
235 |
2021 |
795 |
1027 |
1822 |
787 |
1001 |
1788 |
43 |
16 |
59 |
103 |
33 |
136 |
169 |
94 |
263 |
640 |
1028 |
1668 |
128 |
283 |
411 |
Jedwali: 1.4.2.2 MATOKEO YA UPIMAJI KIDATO CHA NNE TOKA 2019 HADI 2021
MWAKA |
WALIOSAJILIWA |
WALIOFANYA |
DARAJA I |
DARAJA II
|
DARAJA III |
DARAJA IV |
DARAJA O |
||||||||||||||
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
WV |
WS |
JML |
|
2019 |
994
|
1483
|
2481
|
904
|
1381
|
2285
|
9 |
0 |
9 |
83 |
22 |
105 |
123 |
52 |
175 |
408 |
579 |
987 |
104 |
264 |
368 |
2020 |
1054
|
1534
|
2588
|
973
|
1454
|
2427
|
24 |
6 |
30 |
111 |
37 |
148 |
160 |
80 |
240 |
333 |
606 |
939 |
41 |
90 |
131 |
2021 |
1205
|
1583
|
2788
|
1082
|
1471
|
2553
|
28 |
0 |
28 |
35 |
98 |
133 |
79 |
193 |
272 |
708 |
404 |
1112 |
66 |
177 |
243 |
.
Elimu ya Ufundi Stadi
Wilaya ina Vituo viwili vya Elimu ya Ufundi Stadi; Matogoro na Luagala Mission. Vijana wanaomaliza darasa la VII wanayo fursa ya kujiunga na vituo hivi vya ufundi stadi vilivyopo Matogoro na Luagala Mission na kupata mafunzo ya ufundi wa useremala, uashi na sayansi kimu. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni idadi ya wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi imepungua kutoka wanafunzi 41 mwaka 2016 hadi wanafunzi 25 mwaka 2020. Kuna changamoto anuai zinazosababisha hali hiyo ikiwemo upungufu/ukosefu wa vifaa/zana za kufundishia na kujifunzia, rasilimali fedha na walimu wenye ujuzi na taaluma katika fani zinazofundishwa.
Kutokana na mahitaji makubwa ya Elimu ya Ufundi Stadi kwa vijana na watu wazima hususani wanaomaliza darasa la VII, kidato cha IV na VI hata vyuo vikuu, Halmashauri ina mpango wa kufanya maboresho makubwa katika Kituo cha Ufundi Stadi Matogoro ili kiweze kufundisha fani za useremala, uashi, sayansi kimu, uhunzi, umeme na kompyuta. Lengo ni kuwawezesha vijana na watu wazima wengi wapate maarifa, stadi na ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri. Halmashauri tunaamini njia mojawapo ya kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi wetu ni kuwawezesha kupata ujuzi na maarifa kupitia elimu ya ufundi stadi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa