Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuratibu ziara ya mafunzo kwa Wataalamu wa Halmashauri na Madiwani kujifunza ujuzi ambao utaleta tija kwa wananchi wake.
Mhe.Simbachawene ameyasema hayo Juni 10, 2025 mara baada ya kusalimiana nao katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alipokuwa katika ziara yake yake kikazi mkoani humo.
"Nikupongeze Mkurugenzi kwa kuwatoa madiwani kutoka Mtwara mpaka Simiyu kujifunza ni jambo la msingi na halina mwisho, katumieni ujuzi huu kuibadilisha Tandahimba na Mkoa wa Mtwara" Mhe.Simbachawene.
Aidha, amewasisitiza madiwani kujifunza na kukubali kubadilika kwa maslahi ya wananchi wa Tandahimba
Ninaufahamu Mkoa wa Mtwara na Tandahimba sio masikini ina uwezo mkubwa ni wepesi wa kupokea mabadiliko, Msikilizeni Mkurugenzi atawafikisha mbali" Mhe.Simbachawene
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi amewashukuru kwa kuona umuhimu wa kuja kujifunza katika Mkoa huo na kuwasisitiza kuutumia vyema ujuzi watakaoupata kwa manufaa ya wananchi wa Tandahimba.
Kamati ya fedha wamefanya ziara ya mafunzo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Maswa Mkoani Simiyu kujifunza kilimo cha Mkataba(Contract Farming) Uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo na Uendeshaji bora wa kampuni Mahususi ya Halmas
hauri (SPV).
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa