TAARIFA YA IDARA YA AFYA JULAI - SEPTEMBA 2022
Halmashauri ina jumla ya vituo 46 vya kutolea huduma za afya. Katika vituo hivyo kuna Hospitali 1 inayomilikiwa na serikali, vituo vya afya 3 kimoja kati ya vituo hivyo kinamilikiwa na shirika la dini la Roman Catholic na vituo 2 vinamilikiwa na serikali.Pia kuna zahanati 42, zahanati 32 kati ya hizo zinamilikiwa na serikali na 10 zinamilikiwa na watu binafsi.Pia kuna maduka ya dawa muhimu 105 yanayomilikiwa na watu binafsi na phamasi 2 za watu binafsi.
Hali ya dawa
Hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya vinavyomilikiwa na serikali inaridhisha.Uwepo wa dawa (Tracer Medicine) ni 97%, Halmashauri imekuwa ikihakikisha kuwa kila kituo kinakuwa na dawa za ( Oxtocin & Magnesium Sulphate ) kwa ajili ya kuzibiti kifafa cha mimba kwa wajawazito na utokwaji wa damu kwa wingi baada ya kujifungua. Vituo vyote vinapatiwa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwepo fedha ya ruzuku za madawa zinazotumwa bohari ya madawa (MSD), fedha za uchangiaji huduma za afya na Bima ya Afya (NHIF), CHF na fedha za mfuko wa pamoja wa wafadhili ( Basket Fund)..
Mapokezi ya Vifaa Tiba
Ujenzi wa tanuri la kisasa la kuchomea taka Hospitali ya Wilaya
Halmashauri kupitia Wizara ya Afya imepata msaada wa ujenzi wa Tanuri la kisasa ambalo litakuwa linatumia umeme katika uchomaji wa takataka. Ujenzi wa tanuri hilo unaendelea katika Hospitali ya Wilaya’HIGH TECH INCINERATOR’
Hali ya watumishi
Idara ya Afya inakabiliwa na upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali kwa kiwango cha asilimia 62.8% wanaohitajika ni 780 na waliopo ni 290 ambao ni sawa na asilimia 37.18%. Idara ya Afya imepokea jumla ya watumishi wapya 4 wengine kuziba pengo la watumishi wawili ambao hawakuripoti mwanzo
Mapambano dhidi ya ukimwi
Kwa sasa maambukizi ya ukimwi ni 1.6%. Katika kuthibiti na kuzuia maambukizi mapya Halmashauri inaendelea kutoa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa VVU. Aidha Halmashauri bado inaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga na maambukizi ya VVU kwa wananchi wasio na VVU pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maabukizi mapya kwa wananchi wanaoishi na VVU pamoja na kutoa tiba kinga kwa makundi hatarishi ikiwemo wanawake wanaojiuza na watu wanaoishi na wenzi walioathirika. Pia halmashauri inatoa dawa na ushauri kwa ajili ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto. Halmashauri ina jumla ya vituo 13 vinavyotoa huduma za CTC ikiwemo ushauri nasaha na upimaji wa VVU, upimaji wa kinga za mwili (CD 4).Katika kipindi cha Julai -Septemba 2022 jumla ya watu 4698 walipima VVU na kati yao waliokutwa na maambukizi ni 97 ambao ni sawa na asilimia 2.1%.
Taarifa ya upimaji na ushauri nasaha wa VVU
CHINI YA MIAKA 14
|
WALIOKUTWA NA MAAMBUKIZI
|
JUU YA MIAKA 14
|
WALIOKUTWA NA MAAMBUKIZI
|
||||||||||
JUMLA WALIOPIMA
|
ME
|
KE
|
ME
|
KE
|
JUMLA
|
JUMLA WALIOPIMA
|
ME
|
KE
|
ME
|
KE
|
JUMLA
|
||
32
|
15
|
17
|
1
|
2
|
3
|
4666
|
2190
|
2476
|
52
|
42
|
94 |
||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mapambano dhidi ya Malaria.
Katika kupambana na ugonjwa wa malaria idara ya afya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga na maambukizi kwa njia mbalimbali ikiwemo usafi wa mazingira na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viatilifu. Jumla ya waliopima Malaria walikuwa 36,581 ambapo wanaume walikuwa 15,565 na wanawake walikuwa 21,016, waliokutwa na maambukizi ya malaria walikuwa 18,470 kati yao wanaume walikuwa 8,103 na wanawake walikuwa 10,367 sawa na asilimia 50%. Wajawazito waliopewa vyandarua walikuwa 1,908 na watoto waliopewa vyandarua walikuwa 2,406 .
Huduma za maabara
Katika kipindi cha Julai -Septemba jumla ya chupa 564sawa na 87% za damu zilikusanywa kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji damu ikiwemo wajawazito, watoto na wagonjwa wengine wenye uhitaji wa damu.Pia huduma zingine za upimaji wa vipimo mbalimbali zilitotolewa ikiwemo magonjwa ya kuambukiza na ya siyo ya kuambukiza.
mengineyo.
Huduma za chanjo
Katika kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo Halmashauri imekuwa ikiendelea kutoa huduma za chanjo kwa ajili ya kukinga watoto dhidi ya magonjwa ya pepopunda, kifaduro, dondakoo, kichomi, kifua kikuu, kupooza na kuharisha. Lengo la chanjo Kitaifa ni kuwachanja watoto zaidi ya asilimia 90% katika robo hii huduma za chanjo zilizotolewa ni kama ifuatavyo.
Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya pili
Tarehe 1-4/9/2022 kulifanyika kampeni ya chanjo ya Polio awamu ya pili kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano lengo la Halmashauri ilikuwa ni kuchanja watoto 40,607 lakini ilifanikiwa kuchanja 46,249 sawa na asilimia 113%.
Chanjo ya Uviko
Katika kipindi cha Julai hadi September jumla ya watu 67,536 walipatiwa chanjo ya Uviko kati yao wanaume 26,338 na wanawake 41,198.
Hali ya mfuko wa afya ya jamii. (CHF)
Julai – Septemba 2022 ,tumefanikiwa kusajili kaya 99 zilizojiunga na iCHF zenye wanachama 495 mpaka sasa kuna jumla ya kaya 1,378 zilizojiunga na iCHF zenye wategemezi 6,627 ambazo ni sawa na 4 % lengo ni kuandikisha 32,532 kati ya kaya 65,064 ambazo ni sawa na asilimia 50% ya kaya zisizotumia Bima ya Afya (NHIF).
Huduma Za Lishe
Shughuli za lishe zilizofanyika kwa robo hii ya kwanza ni udhibiti wa matatizo makuu ya Lishe nchini ambayo ni upungufu wa madini joto, utoaji wa nyongeza ya Vitamini A, na utambuzi wa watoto utapiamlo pamoja na matibabu ya utapiamlo mkali.
Katika robo hii tumefanikiwa kutoa elimu ya ulishaji watoto wachanga na wadogo kupitia vituo vyetu vya kutolea huduma za Afya ngazi ya jamii. Jumla ya wazazi/walezi 14,162 waliweza kufikiwa ikiwa ni mapambano endelevu dhidi ya udumavu. Aidha elimu juu ya Lishe bora kwa watu wote inaendelea kutolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
Jumla ya walengwa wa Vitamini A kwa robo hii walikuwa 3,570 na waliopatiwa Vitamini A ni 3,932 sawa na 110%.
Walengwa wa utapiamlo mkali ni kwa robo hii ni 45. Jumla ya watoto waliobainika ni 28 waliopatiwa matibabu na kupona ni 27. Mtoto 1 anaendelea na matibabu.
Ukaguzi wa chumvi zenye madini joto ulifanyika katika maduka ya Tandahimba na Kitama, jumla ya sampuli 23 zilipimwa kutoka katika maduka madogo, sampuli 18 (78%) zilikua na madini joto na sampuli 5(22%) hazikuwa na madini joto.
Aidha tulipima chumvi kwa ngazi ya kaya kwa kutumia wanafunzi wa shule ya msingi Matogoro. Jumla ya sampuli 176 zilipimwa. Sampuli 158 (90%) Zilikua na madini joto ya kutosha na sampuli 18(10%) hazikuwa na madini joto kabisa.
Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji dunia kuanzia tarehe 1-7/08/2022 ambapo elimu ya ulishaji wa watoto wachanga na wadogo ilitolewa kupitia vituo vyote vya kutolea huduma za Afya na Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii.Jumla ya wazazi/walezi 9,196 (70 %).
Imeandaliwa na
Dr.Grace Paul
Kny:Mkurugenzi Mtendaji (W)
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa