Mkaguzi Mkazi -Mkoa wa Mtwara (CEA) Andindilile Mwabwanga ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kupata hati hati safi baada ya kupitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Mwabwanga ameyasema hayo kwenye baraza maalumu la Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema matokeo mazuri ya Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali hayakuja tu hivihivi .
"Tandahimba kuendelea kupata hati safi mara tano mfululizo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Madiwani, Mkurugenzi na Wataalamu wake katika kuhakikisha mambo yanaenda" Mhe.Baisa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewasisitiza kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na CAG ili Halmashauri hiyo iendelee kufanya vizuri.
"Maelekezo na mapendekezo yaliyotolewa hasa ya Miradi yafanyiwe kazi kwa wakati kwa siku hizi 13 zilizobaki hadi kufikia tarehe 30 Juni miradi iwe imekamilika" Kanali Mntenjele
Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kwa kipindi cha Miaka mitatu ilipanga kukusanya kiasi cha Tsh.Bilioni 16 ambapo imekusanya kiasi cha Tshs.Bilioni 15 sawa na zaidi ya 90% ya makusanyo .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa