Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Zoezi la sensa ya majaribio katika kijiji cha Bandari Kitongoji cha Ruvuma kata ya Michenjele Wilaya ya Tandahimba limekamilika ambapo kaya 175 na nyumba 197 zimehesabiwa
Miongoni mwa nyumba ambazo zimehesabiwa kwenye sensa ya majaribio kijiji cha bandari
Mratibu wa sensa Wilaya ya Tandahimba ndugu Karimu Mputa amesema zoezi hilo limekamilika Septemba 19,2021 kwa ushirikiano mkubwa wa kamati ya sensa Mkoa, Wilaya na Taifa sambamba na wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wachukua taarifa
Mratibu wa Sensa Wilaya ya Tandahimba ndugu Karim Mputa akielezea jambo
“Zoezi limekamilika kwa mafanikio makubwa kaya zote 175 na nyumba 197 zimehesabiwa ,wananchi wametoa ushirikiano kwa makarani ambao wamepita kwenye kaya zao ,tunashukuru kamati za sensa ngazi ya kata na kijiji kwa kufanya uhamasishaji kwa wananchi ,tunaamini zoezi hili litaleta dira nzuri kwa sensa ya mwaka 2022,”amesema Mratibu
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho
Aidha amesema sensa ya majaribio katika kijiji hicho wameweza kuhoji kaya zote,kuhesabu nyumba zote na kusajili anwani zote za makazi kwa kutumia mfumo wa Tehama (CSEntry na Napa) kufanya kazi kwa ufasaha
Karani wa sensa akichukua taarifa kwa mkazi wa kijiji cha bandari na kujaza moja kwa moja kwa kutumia kishikwambi
Sensa ya majaribio katika kijiji cha Bandari ilianza Septemba 8,2021 na kukamilika Septemba 19,2021 ambayo itatoa dira kwa sensa itakayfanyika Agosti 2022
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa