Mkutano wa baraza la Madiwani Robo ya tatu (Januari -Machi 2024) Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba umefanyika Leo Mei 17, 2024 na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Baisa Baisa ambaye katika hotuba yake kwenye Baraza hilo amesisitiza uwepo wa ziara za madiwani kwa ajili ya kujifunza shughuli za Maendeleo nje ya Wilaya ya Tandahimba ili kupitia ziara hizo Madiwani waweze kuzifanyia kazi kwa manufaa ya Halmashauri na Wananchi wake.
Kwa Upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Edith Shayo amesisitiza Baraza hilo la Madiwani kuchagua kwa uangalifu maeneo ya kujifunza.
"Nendeni mkajifunze na mnapopanga kwenda chagueni maeneo ambayo yataleta matokeo chanya na tija kwa Wananchi na sio kwenda tu kwa sababu ni ziara" Edith.
Mkutano wa Baraza la Madiwani umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Mkuu wa Wilaya pamoja na Viongozi mbalimbali Wa Halma
shauri.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa