Kamati ya fedha wamefanya ziara ya mafunzo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Maswa Mkoani Simiyu kujifunza kilimo cha Mkataba(Contract Farming) Uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo na Uendeshaji bora wa kampuni Mahususi ya Halmashauri (SPV).
Katika Ziara hiyo Madiwani hao wamefika katika Kiwanda cha Kuchakata Pamba na Mpunga cha Allience Ginneiry ambacho kinafanya vizuri katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Akizungumza katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema kupitia kujifunza kilimo cha Mkataba ambacho Kampuni inakuwa na mkataba na Mkulima kwa lengo la kumpatia pembejeo za kilimo na baada ya kuvuna anauza mazao hayo kwa Kampuni hiyo .
"Mfumo huu wa kiwanda utawasaidia wakulima wetu wa Tandahimba katika zao la Korosho kwani kupitia Kilimo cha Mkataba kinamsaidia mkulima kwanza kupata pembejeo lakini anakuwa na soko la uhakika kwa sababu kazi ya kutafuta soko ni ya Mwenye kiwanda" Baisa.
Aidha, katika Uendeshaji bora wa Kampuni Mahususi ya Halmashauri Wilayani Maswa madiwani hao wametembelea na kujifunza katika Kampuni ya Ng'hami inayomiliki viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Uzalishaji wa Chaki ambacho kinaongoza kwa uzalishaji wa chaki Nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo Madiwani wameambatana na Wataalamu wa Halmashauri, na Mmiliki wa kiwanda cha Kubangua korosho cha TDC Bosco Mamangaya ambae amesema atatumia ujuzi alioupata Bariadi kuwasaidia wakulima wa Korosho Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa