Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasistiza Wakulima wa Tandahimba kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa zao la mbaazi kwenye mfumo huu wa mwaka 2023/2024
Akizungumza na Viongozi wa Vyama vya msingi (Amcos) Watendaji wa Kata na Madiwani kwa nyakati tofauti katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Agosti 9,2023 amesema kuwa zao la Mbaazi linaanza rasmi katika msimu huu kuuzwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo mkulima atafaidika na zao lake
" Zao hili halikuwepo katika mfumo wa stakabadhi ghalani lakini kwenye msimu huu wa mwaka 2023/2024 litaanza rasmi hivyo wahimizeni Wakulima katika maeneo yenu kupeleka Mbaazi zao katika Amcos zilizopo katika maeneo yao kuepuka uuzwaji holela ambao unamkandamiza mkulima," amesema Dc Sawala
Naye Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika TANECU Ndg.Mohamed Mwing'uku amesema kuwa tayari vifungashio vipo tayari katika Amcos hivyo Wakulima wazingatie Ubora kwa kuepuka kuchanganya vitu ambavyo sio mbaazi wakati wa kuziandaa ili ziweze kuuzwa kwa bei ya juu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa