Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Tandahimba (CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo DCI.Mariam Mwanzalima imefanya ziara ya siku mbili ikitembelea na kukagua miradi ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.
Mkurugenzi Mtendaji DCI.Mariam Mwanzalima amewasisitiza wasimamizi wa miradi katika maeneo husika kuongeza kasi ya ujenzi iweze kukamilika kwa wakati ili itoe huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
Katika ziara hiyo Menejimenti imekagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo na kutoa maelekezo mahususi ya namna bora ya kukamilisha miradi hiyo kwa viwango vilivyowekwa.
Aidha, Miradi iliyotembelewa na CMT ni pamoja na sekta ya Elimu ikijumuisha ujenzi wa Madarasa, Nyumba za walimu na Matundu ya Vyoo, Sekta ya Afya na sambamba na Sekta ya Mifugo .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa