Benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) tawi la Tandahimba imemtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba DCI.Mariam Mwanzalima kwa lengo la kumpongeza na kusherehekea pamoja katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa ambayo ni Septemba 15, 2025 ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kuanzishwa na kuendelezwa kwa benki hiyo.
Katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake, uongozi wa Coop Bank ukiongozwa na Meneja wa Tawi la Tandahimba Salumu Halfani umemkabidhi zawadi maalum kama ishara ya pongezi na shukrani.
DED Mwanzalima ni miongoni mwa waanzilishi wa Coop Bank na amekuwa mjumbe wa bodi ya mpito tangu kuanzishwa kwake mnamo Mwaka 2024,
nafasi iliyomuwezesha kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya benki hiyo.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ni mwanahisa wa Benki hiyo ya Ushirika ambapo viongozi hao wamejadili mambo mbambali ikiwemo namna ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo nafuu kwa wakulima na Wajasiriamali wadogo, elimu ya fedha, na huduma za kisasa za kibenki.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji huyo ameishukuru Coop Bank kwa kutambua mchango wake na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya wananchi wa Tandahimba na taifa kwa ujumla.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa