Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kiasi cha shilingi 212,234,000 zimetumika kuhaulishwa kwa kaya 6175 kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kwa vijiji 88 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Mratibu wa TASAF Tandahimba Ismaely Mbilinyi(aliyesimama) akizungumza na wanufaika wa kijiji cha Mkonjowano
Akitoa tathmini ya zoezi la uhaulishaji ambalo limefanyika kwa vijiji 88 Mratibu wa TASAF Wilaya ya Tandahimba ndugu Ismaely Mbilinyi amesema kuwa zoezi hilo limefanikiwa na kukakamilika kwa muda uliopangwa kwa malipo ya mwezi Mei-Juni ,2021
Amesema shilingi 213,304,000 zilitakiwa ziwafikie walengwa 6214 kwa vijiji 88 ambavyo vipo kwenye mpango lakini shilingi 1,070,000 za walengwa wa kaya 39 hazikuwafikia kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwa mbali na maeneo yao wakati wa malipo,kaya 8 walengwa wamefariki dunia na walengwa 10 wamefuzu katika mpango huo
Walengwa wakiwa kwenye kituo cha malipo ambapo pia walipata huduma ya elimu na chanjo ya Uviko-19
“Tunashukuru zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa,walengwa wa kaya ambazo zina wanafunzi wahakikishe wanapatiwa mahitaji muhimu ya shule,lakini pia tunawaomba walengwa wakati wa zoezi la malipo wawepo katika vituo vyao ili walengwa wote waweze kupata malipohayo kwa wakati ,”amesema ndg Mbilinyi
Mratibu amesema miongoni mwa changamoto ambazo wamekutana nazo ni pamoja na majina ya walengwa kutofautiana na namba zao za usajili wa vitambulisho vya Taifa(NIDA)
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa