Na Kitengo cha Mawasiliano
Wito umetolewa kwa viongozi wa dini ,wazee maarufu na viongozi wa Mila Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuendelea Elimu kwa jamii inayowazunguka ili kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto
Akitoa Wito huo Novemba 18,2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Halmasahauri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg,Robert Mwanawima amesema washiriki hao wana nafasi katika jamii inayowazunguka ili kupinga ukatili
“Vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii yetu upo ambapo mna nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii ili kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia kila mmoja katika nafasi yake,’amesema Ndg.Mwanawima
Naye Mratibu wa Dawati la Jinsia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Neema Shungu akifafanua hali ya Ukatili kwa wanawake wa Tandahimba amesema wanawake wanaathirika na ukatili wa Kisaikolojia,Kihisia,kimwili,kiuchumi na kingono
Aidha naye Afisa Ustawi wa Jamii Bi.Gift Limbanga amesema kutokana na elimu wanayotoa kuhusu haki za watoto kwa kiasi kidogo jamii imeelimika kuhusiana na Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji wa watoto
Nao washiriki wa kikao kazi hicho kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii kushirikiana na viongozi wa vitongoji waliopo katika maeneo yao ili kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa