Na.Kitengo cha Mawasiliano
Wataalamu na Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Siha kutoka Mkoani Kilimanjaro wamefika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Kwa ajili ya kujifunza namna bora ya ukusanyaji wa Mapato kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani sambamba na Mfuko wa Elimu ambapo vyote hivyo vinatekelezwa kwa ufanisi katika Wilaya ya Tandahimba.
Awali akizungumza katika Kikao Cha ndani Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Dkt.Christopher Timbuka amesema wameona ni vema kuja kujifunza Tandahimba Kwa kuwa ni Wilaya inayofanya vizuri kwa ukusanyaji wa Mapato kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani .
Katika kipindi Cha Mwaka wa Fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imekusanya Mapato kiasi Cha Tsh.Bilioni 6.7 sawa na 120.98% ya Makisio ya Bajeti ambayo ilikuwa Tsh. Bilioni 5.5.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa