Na Kitengo cha Mawasiliano
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amefanya ziara ya siku moja Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo amekagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
Akiwa katika ziara yake Agosti 13,2023 amekagua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Kubangua Korosho cha Organic Growth,ujenzi wa kituo cha afya Kitama,ujenzi wa shule mpya ya msingi Mambamba na amezindua mradi wa Maji Kitama
Aidha Waziri Mkuu ameipongeza miradi hiyo na kusistiza kuwa nia ya Serikali ni kuona miradi inatekelezwa kwa wakati na ubora unaotakiwa
Akizungumza na wananchi kwenye Uwanja wa Majaliwa Waziri Mkuu amewasistiza wakulima kujikita katika kuongeza thamani ya korosho kwa kuzibangua na kuanzisha viwanda vya ubanguaji
Hata hivyo amesistiza hatua kali zichukuliwe kwa yoyote atakayebainika kuhusika kuhujumu pembejeo za wakulima ambazo zimetolewa na Serikali ili ziwasaidie wananchi kuongeza uzalishaji
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa