Na. Kitengo cha Mawasiliano
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa vya kidigitali sambamba na kuwasimamia wanapovitumia ili kuwalinda na vitendo vya ukatili
Hayo yamesemwa Juni 15,2023 na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya yaTandahimba Ndg.Francis Mkuti katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Kiwilaya ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba yameadhimishwa katika Kata ya Nambahu
"Uangalizi na ukaribu wakati wa matumizi ya vifaa hivi vya kidigitali kama vile simu janja wa kuzingatiwa ili kuwaepusha watoto na mitandao ya kijamii ambapo imechukua nafasi ya malezi ambayo haipo kwa nia njema badala yake mtumie muda kuzungumza nao ili kuwapa elimu,tumieni kupiga namba 116 bure kutoa taarifa za ukatili wa mtoto ," amesema Ndg. Mkuti
Katika taarifa yake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wialaya ya Tandahimba Ndg.Aloyce Massau amesema zipo mila na mifumo inayopelekea wazazi kutengana na kusababisha watoto kukosa haki zao za msingi na kupelekea kuwa na wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika maisha magumu
Jumla ya Kamati 30 za ulinzi na usalama wa mtoto zimeundwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ili kuendelea kutoa elimu kwa ,kauli mbiu ya mwaka huu "Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa Kidigitali"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa