Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka wazazi na walezi wenye watoto chini ya miaka mitano kuhakikisha wanapata chanjo ya Polio awamu ya nne ili kuwakinga watoto na ugonjwa wa Polio
Amesema hayo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) kilichofanyika Novemba 25,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo amesema kuwa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Polio Awamu ya nne itaanza rasmi Disemba 1 hadi Disemba 4,2022
“Ili kuhakikisha watoto wanakingwa na ugonjwa wa Polio Serikali imeamua kurudia zoezi la Kampeni ya Polio awamu ya nne ambalo litafanyika pia katika Wilaya yetu,’amesema Dc
Lengo la Kampeni ya awamu ya nne ni kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano ambao hawakupata chanjo ya Polio awamu ya tatu wanapata na ambao walichanjwa awamu ya tatu wanachanjwa tena
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Katika Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya nne inatarajia kuwafikia watoto 46,249
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa