Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakao jihusisha na uuzaji wa pembejeo feki na watakao gawa pembejeo za ruzuku kwa wasiohusika
Ameyasema hayo leo Mei 31,2022 viwanja vya shule ya msingi Amani katika mkutano wa hadhara ambapo ametoa utaratibu wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima
“Wale wanaotaka kujihusisha na uuzaji wa pembejeo feki waache mara moja,kufanya hivyo ni kosa la uhujumu uchumi na hatutakuvumilia uhujumu uchumi wa Tandahimba lakini pia pembejeo hizi zimetolewa kwa wakulima ambaye atatoa pembejeo hizi kwa asiyehusika naye tutamchukulia hatua,”amesema Dc Sawala
Amesema zoezi la ugawaji wa pembejeo za ruzuku utakuwa wa wazi ili kila mkulima ambaye anastahili aweze kupata pemjeo hizo na kusistiza kuwa kila mkulima ahakikishe shamba lake lipo safi ili pembejeo hizo zifanye kazi ipasavyokuongeza uzalishaji
Aidha amesema kuwa tayari pembejeo hizo zimeanza kuwasili katika maghala ambapo katika mgao wa pembejeo hizo wamezingatia uzalishaji wa msimu uliopita wa mwaka 2021/2022
Katika mgao wa Jumla tutapewa tani 3769.709 za Salfa ya unga,Viuatilifu vya kudhibiti mbu wa korosho tutapewa lita 44334,Viuatilifu vya kudhibiti vidungata tutapewa lita 14777,Viuatilifu vya kudhibiti ubwili unga na braiti tutapewa lita 132995,viuatilifu vya kudhibiti ubwili unga pekee tutapewa lita 29555 na mabomba ya kupulizia 517 ambapo pembejeo hizo zinaendelea kuwasili katika maghala
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa