Na Kitengo cha Mawasiliano.
Watumishi wa Afya ngazi ya Wilaya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa kidigitali wa ufanyaji wa usimamizi shirikishi ( AFYASS-Afya Supportive Supervision System).
Akizungumza kwenye mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yamehitimishwa leo Disemba 15,2023 kwenye ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba Mwezeshaji Ndugu.Edward Ngonyani amesema kuwa mfumo huo umelenga kuondokana na utumiaji wa karatasi.
Aidha amesema umuhimu wa mfumo huo ni kuweza kuratibu shughuli za usimamizi na tathmini ya taarifa na mifumo ya Afya,kufanya tathmini ya maazimio ya simamizi shirikishi zilizofanyika na kuwezesha kukabiliana na changamoto za utoaji wa huduma za Afya.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na UNICEF lengo ni kuwajengea uwezo ili kuweza kutumia mfumo huo mpya.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa