Na Kitengo cha Mawasiliano.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa kujisajili kwenye mfumo wa kupima utendaji kazi wa watumishi wa umma( PEPMIS/PIPMIS)
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo mwezeshaji Ndugu.Raphael Mputa amesema kwenye mfumo huo watumishi wote watajaza taarifa zao za kiutumishi na fomu za upimaji wa kazi zao .
Aidha mafunzo hayo yameanza leo Novemba 28,2023 kwa watumishi wote wa Ofisi Kuu na yatahitimishwa Disemba 2,2023 ambapo yatawafikia watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba .
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa