Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amewaongoza watumishi kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere
Zoezi la usafi limefanyika leo Oktoba 14,2023 ikiwa ni miaka 23 ya Hayati baba wa Taifa ambapo watumishi wamekuja kufanya usafi lakini p[ia kupima afya na kuchangia damu ili ziweze kuwasaidia watanzania wenye uhitaji
“Leo tunamuenzi Hayati baba wa Taifa kwa kufanya usafi,Hayati baba wa Taifa aliamini katika Utu ni kazi nasisi tunamuenzi kwa kufanya kazi ya usafi lakini pia kupima afya na kuchangia damu,”amesema Mkurugenzi
Naye Bi.Jane Mallongo Mkuu wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu na Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amesema kuwa watumishi wamehamasika na kushiriki katika zoezi la usafi ikiwa ni siku ya Kumbukizi ya Hayati baba wa Taifa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa