Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru watumishi na wananchi wameshiriki michezo mbalimbali sambamba na usomaji wa Insha kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari
Michezo hiyo imefanyika Disemba 8,2022 katika Kiwanja cha Mpira shule ya Msingi Amani iliyopo Kta ya Tandahimba ambapo michezo mbalimbali ilikuwepo
Akizungumza katika eneo hilo Katibu Tawala Ndg.Juvenile Mwambi amesema kuwa michezo ni afya hivyo kuelekea miaka 61 ya Uhuru muhimu kuimarisha afya ili kuendelea kuleta maendeleo
“Michezo ni afya hivyo kuelekea katika maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru tumekuja kuadhimisha kwa kufanya michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zetu lakini pia kusikiliza wanafunzi insha ambazo zinazungumzia miaka 61 ya Uhuru wetu,”amesema Das
Katika upande wa Insha wananfunzi sita wa shule ya msingi watatu na Sekondari watatu waliibuka washindi baada ya kuwasilisha insha zao na kusikilizwa na kamati maalum ambapo wanafunzi hao watakabidhiwa zawadi zao katika Kongamano la maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru yaytakayofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Disemba 9,2022
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa