Na Kitengo cha Mawasiliano
Watumishi katika Wilaya ya Tandahimba wamepewa elimu kuhusu kanuni na mfumo mpya wa kikokotoo cha mafao ya pensheni itakayotolewa kwa watumishi mara baada ya kustaafu
Akiongoza mafunzo ya Utoaji Elimu katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri Agosti 29,2022 Meneja wa kanda Ndugu.Sayi Lulyalya amesema lengo ni kuelekeza namna ya utoaji wa mafao kwa kutumia kikokotoo kipya kulingana na kanuni mpya iliyoelekezwa na PSSSF
Amesema kanuni hiyo ilitangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu eProf. Jamal Katundu kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mnamo Mei 14, 2022 kuhusu mapendekezo ya mafao ya wastaafu illiyoombwa na TUCTA Mei mosi, 2022.
Kanuni mpya inaongeza kiwango cha mkupuo kutoka asilimia 25 iliyolalamikiwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 ambapo itafanya wanachama wote wa mifuko kunufaika na ongezeko hilo pia malipo ya mkupuo yatapanda kwa asilimia 81 na malipo ya pensheni yataongezeka kwa asilimia 19 ya wanachama.
Kikokotoo kipya kimetolewa kwa ajili ya kupunguza changamoto zilizokuepo katika mfumo wa awali na kuwataka washiriki kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kuboresha zaidi mfumo wa utoaji wa mafao kwa wastaafu.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa