Na.Kitengo cha Mawasiliano.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepatiwa Elimu ya Uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili kunufaika na Uwekezaji huo.
Elimu hiyo imetolewa leo Februari 20,2024 na Wawezeshaji kutoka Benki Kuu ya Tanzania( BOT) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Akitoa elimu hiyo Mwezeshaji Ndugu.Benn Mgowole amesema faida za kuwekeza katika Dhamana za Serikali ni Salama kwani Serikali haitarajiwi kukiuka mategemeo ya wadai wake wakati wa malipo,Dhamana za Serikali zinaweza kutolewa kama Dhamana kwa ajili ya kupata mikopo katika taasisi za fedha nchini lakini pia zina viwango vya riba vinavyoridhisha.
Dhamana ya Serikali ni aina ya Uwekezaji unaotegemea mpango wa ndani wa ukopaji wa Serikali ambapo mwekezaji anatoa mkopo kwa Serikali kwa malipo ya kuponi iliyokubaliwa na baada ya muda wa dhamana kuisha kiasi cha awali cha uwekezaji hurudishwa kwa mwekezaji kwa asilimia 100.
Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiendesha minada ya Dhamana za Serikali kulingana na Mpango wa Ukopaji wa Serikali kutoka Masoko ya mitaji ya ndani ya nchi bila kuathiri mikopo kwa sekta binafsi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa