Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeleta Mtaalamu wa Mfumo wa Ununuzi kwa Njia ya Mtandao (NeST) kwa ajili ya kuwafundisha Watumishi mbalimbali wa Halmashauri hiyo ili waweze kutekeleza Miradi ya Maendeleo kupitia Mfumo huo.
Akifungua mafunzo hayo Leo Januari 22, 2024, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joshua Mgoli amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo na kuongeza kuwa Hakuna manunuzi yoyote yatakayofanyika nje ya Mfumo wa NeST , akiwasisitiza wataalamu kuyafanyia kazi ili shughuli zote za Maendeleo zinazotekelezwa kwa Mfumo huo zisikwame.
"Tuwe makini na Mafunzo haya yakasaidie taasisi yetu katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo kupitia Mfumo huu, hatutarajii baada ya Mafunzo haya sababu ya kukwama kwa Miradi iwe ni NeST"Mgoli
Jumla ya Watumishi 512 wanatarajia kupata Mafunzo hayo kwa Muda wa Siku Saba katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa