Na Kitengo cha Mawasiliano
Watu 8705 wamechanja chanjo ya Uviko-19 kwa muda wa siku mbili katika Kampeni mahususi ya kuhamasisha chanjo hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Uhamasishaji huo umetolewa na timu ya Mziki Mnene ambapo ilipita baadhi ya vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kutoa elimu ya chanjo ya Uviko-19 na burudani kuanzia Julai 30-31, 2022
Idadi hiyo imepatikana kwa siku mbili ambapo wananchi wamejitokeza kuchanja kwa siku ya kwanza watu 3999 walipata chanjo ya Uviko – 19 na siku ya pili watu 4706
Wananchi wakichanja chanjo ya Uviko - 19 katika kata ya kitama
Aidha baada ya kupita katika vijiji walihitimisha kwa kufanya tamasha la uhamasishaji katika viwanja vya shule ya msingi Amani ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kuchanja chanjo ya Uviko-19
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa