Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Kiwilaya kwa kuwapima afya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Mji mpya sambamba na utoaji wa elimu ya lishe kwa wapishi wa watoto hao
Zoezi la kuwapima afya watoto hao limefanyika shuleni hapo leo Juni 15,2022 ambapo watoto 94 wamepimwa malaria na kuangalia hali ya macho kati yao watoto 32 wamebainika kuwa na malaria,watoto 13 wamebainika kuwa na tatizo la macho ambapo wote wamepatiwa matibabu
Akizungumzia tukio hilo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tandahimba Ndugu. Aloyce Massau amesema kuwa hatua hiyo ya kuwapima afya imewezesha kufahamu afya zao
“Leo katika kuadhimisha siku hii kiwilaya sisi Halmashauritumeona tuitumiesiku hii kuwapima afya watoto wetu wenye mahitaji maalum,kwasababu watoto hawa wanaishi hapa bweni kwaiyo kwa kuwapima afya tutajua maendeleo yao ya kiafya lakini pia wapishi wanapewa elimu ya kuwaandalia watoto lishe bora kwa kuzingatia makundi matano ya chakula,”amesema Ndg. Massau
Naye Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Thadei Luhumbo amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kuthamini afya za watoto hao ambao huwa wanapata changamoto mbalimbali za kiafya
Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika hufanyika Juni 16 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2022 ni “Tuimarishe ulinzi wa Mtoto,Tokomeza Ukatili dhidi yake,Jiandae Kuhesabiwa”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa