Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Watoto 40428 sawa na asilimia 118 wamechanjwa katika Kampeni ya Kitaifa ya siku nne ya Utoaji wa Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akizungumzia Kampeni hilo Mratibu wa Chanjo Ndg.Juma Makame amesema kuwa lengo la Halmashauri ni kupata watoto 34984 kwa siku nne ambapo kwa siku nne(4) lengo limefikiwa
Kampeni hiyo ilianza Mei 18,2022 ambapo watoto waliochanjwa chanjo ya polio siku ya kwanza 9647 sawa na asilimia 113,siku ya pili Mei 19,2022 watoto 11275 sawa na asilimia 132 ,siku ya tatu Mei 20,2022 watoto 11754 sawa na asilimia 137 na siku ya nne Mei 21,2022 watoto 7752 sawa na asilimia 90.6
“Kampeni hii tulikuwa tunapita nyumba kwa nyumba,vituo vya watoto (awali) ambapo tumeweza kufikia lengo letu , kwa siku tulitakiwa tuwe tunachanja watoto 8562 ili tuweze kufikia lengo la watoto 34248 ambalo tumefikia na tumepita,”amesema Mratibu
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dkt.Grace Paul (wa kwanza upande wa kulia) akiwa pamoja na wataalamu wa afya wakipita nyumba kwa nyumba kuchanja chanjo ya polio
Aidha wananchi kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali kwa hatua za haraka walizochukua ili kuwakinga watoto na madhara kwa kuwapa chanjo ya polio ya nyongeza
Katika kampeni hiyo nyumba ambazo watoto wamechanjwa chanjo ya polio wameweka alama lakini pia zile ambazo hazikuwa na watoto chini ya miaka mitano ziliwekwa alama pia
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa