Na.Kitengo cha Mawasiliano
Watoto wenye umri chini ya miaka mitano 11090 sawa na asilimia 109.24 wamechanja chanjo ya Polio ya matone ikiwa ni siku ya kwanza ya Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio Awamu ya Tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Akitoa takwimu hiyo Septemba 1,2022 Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dk.Grace Paul amesema wazazi na walezi wamehamasika kufika katika vituo vya kutolea huduma ya afya na watoa huduma ya afya kutembelea nyumba kwa nyumba kutoa chanjo ya Polio ili kuwakinga watoto
“Tunameanza chanjo ya polio katika maeneo yetu wazazi na walezi wanajitokeza kuchanja watoto wao lakini pia watoa huduma ya afya wanatembelea nyumba hadi nyumba zenye watoto chini ya miaka mitano kuwapa chanjo,kwaiyo tumeanza vizuri maana tumepita lengo la siku,”amesema Dk.Paul
Aidha amesema kuwa Katika Kampeni hii Lengo ni kuchanja watoto wasiopungua 40607 kwa siku nne katika Halmashauri ya Tandahimba ambapo lengo la siku ni kuchanja watoto 10152
Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo ya Polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inaendelea ambapo imeanza Septemba 1,2022 na itamalizika Septemba 4,2022
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa