Na Kitengo cha Mawasiliano
Watoa huduma za afya wametakiwa kuratibu huduma bora za mama na mtoto ili kuhakikisha vifo vitokanavyo na changamoto za uzazi na watoto wachanga havitokei katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Ameyasema hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendahi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Raphael Mputa wakati akifungua mafunzo ya Huduma Muhimu kwa Wajawazito leo Septemba 19,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
”Zingatieni mafunzo haya ili kuhakikisha Halmashauri yetu tunaondoa kabisa tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi ,mikakati iliyopo ni kuhakikisha huduma zinapatikana karibu na mwananchi kwa wakati wote,”amesema Ndg.Mputa
Naye Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Dk.Grace Paul ameeleza kuwa changamoto ya uwepo wa vifo vya uzazi lipo katika Halmashauri yetu vikihusisha sababu mbalimbali ikiwemo Wajawazito kuchelewa kupata huduma za kitaalamu
Aidha naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dk.Omary Kilume amesemawatoahudumawakizingatia mafunzo hayo yatawasaidia kupunguza au kuondoakabisa vifo vitokanavyo na uzazi ambapo miongoni mwa sababu ni v kutoka damu nyingi baada ya kujifungua na kifafa cha mimba
Jumla ya Watoa huduma za afya mia moja themanini (180) watapata mafunzo hayo kwa siku tisa ili kuwajengea uwezo katika eneo la mama na mtoto ili waweze kuendelea kutoa huduma bora
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa