Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Watoa huduma idara ya afya ngazi ya Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya katika Halmashauri ya Tandahimba wanatarajia kupewa mafunzo ya lugha za alama ili kurahisisha mawasiliano wakati wa kutoa huduma za afya kwa wenye ulemavu wa kusikia(viziwi)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndg.Said Msomoka amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma kuwasiliana na viziwi wanapokuja kupata huduma
Mkurugenzi Mtendaji ndg.Said Msomoka akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yakavyowasaidia watoa huduma
“Mafunzo haya ambayo watapatiwa watoa huduma yatawasaidia kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kiafya katika vituo vya afya ,”amesema Msomoka
Naye Mratibu wa mradi wa kuboresha mawasiliano wa huduma kwa viziwi katika sekta ya afya ambao unasimamiwa na Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mtwara ndg.Kassim Mchindula amesema kuwa mradi huo utapunguza changamoto mbalimbali za mawasiliano kwa kundi hilo Wilayani Tandahimba
Mkalimani wa lugha za alama akiwafafanulia maelezo kiongozi wa chavita tawi la Tandahimba na
“Viziwi hupata changamoto ya mawasiliano wanapokwenda kupata huduma katika hospitali na vituo vya afya hivyo mradi huu utasaidia kutoa mafunzo ili watoa huduma waweze kuwa na uelewa wa jinsi ya kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia,”amesema ndg. Mchindula
Halmashauri ya Tandahimba ina jumla ya viziwi 3195 kwa idadi ya sensa ya mwaka 2012 ambapo mradi wa mawasiliano utawafikia
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa