Watoa Huduma ngazi ya Vituo vya Afya na Zahanati wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameanza kupatiwa mafunzo ya kutumia mfumo wa kielektroniki (GoTHoMIS Centralized ) ambao una lengo la usimamizi wa shughuli za uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza na watoa huduma ngazi ya vituo vya afya waliohudhuria mafunzo hayo leo Septemba 18,2024 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dkt.Adorat Mpollo amewasistiza kuzingatia mafunzo hayo ili kuboresha huduma za afya na kuongeza ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao
Amesema mfumo huo utawasaidia kurahisisha shughuli za vituo vya kutolea huduma za afya kusimamia uzalishaji na uhifadhi sahihi wa taarifa na takwimu za wagonjwa na magonjwa,mapato na dawa za vituo vya kutolea huduma za afya.
Mafunzo hayo yatatolewa kwa siku nane ( 8) kwa watoa huduma wa vituo vya afya saba (7) na kuhitimisha kwa watoa huduma za afya wa zahanati 29 ambao watapewa mafunzo ya siku nne (4) Katika Ukumbi wa mikutano wa Hospitali wa Wilaya ya Tandahimba.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa