Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama amewataka watendaji wa kata na vijiji kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake waimarishe umoja na ushirikiano ili waweze kuwahudumia wananchi katika maeneo yao
Watendaji wa kata na vijiji kwakifuatilia mafunzo
Ameyasema hayo Januari 20,2022 wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa kata na vijiji yenye lengo la kuwajengea uwezo ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano
Mwezeshaji ndugu Raphael Mputa akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi amesema kuwa mafunzo hayo yataleta matokeo yenye tija kwa watendaji hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taratibu,sheria na miongozo ya utumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi
Watendaji wa kata na vijiji wakiwa kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo katika ukumbi wa mikutano
“Sisi wote ni timu moja ambao tunajenga Halmashauri moja umoja na ushirikiano ni msingi wa utoaji wa huduma bora katika maeneo yenu,msifanye kazi kwa mazoea ninyi ni viongozi mnatakiwa kuwa wabunifu ili kutekeleza wajibu wenu ipasavyo,msimamie utawala bora kwa kufanya mikutano ya katika maeneo yenu ,”amesema Mkurugenzi
Aidha amewasistiza watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika maeneo yao inasimamiwa na kukamailika kwa wakati na ubora,ameeleza kuwa kasi iliyotumika kutekeleza miradi ya Uviko iendelee kutekeleza miradi mingine inayoendelea
Mwezeshaji ndugu Faraji Kulodya akitoa mada ya manunuzi katika mafunzo hayo
Katika mafunzo hayo ya siku moja watendaji wa kata na vijiji wamejengewa uwezo katika mada mbalimbali zilitolewa na wawezeshaji kutoka ngazi ya Halmashauri ya Wilaya
Mwezeshaji ndugu Zuberi Charahani akiwasilisha mada ya mabaraza ya kata na utungaji wa sharia ndogo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa