Na Kitengo cha Mawasiliano
Watendaji Kata Halmashauri ya Wil,aya ya Tandahimba wamesistizwa kuendelea kusimamia na kutekeleza afua za lishe katika maeneo yao
Ameyasema hayo Afisa Tawala Wila ya Tandahimba Ndg.Francis Mkuti wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji afua za lishe ngazi ya Kata kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dc
“Nawapongeza kwa kuendelea kusimamia afua za lishe katika maeneo yenu,nawasistiza msimamie ili shughuli zote za lishe ambazo zinatakiwa kufanyika katika vijiji vyenu zinafanyika ili tuendelee kuwa na watoto wenye afya bora,”amesema Mkuti
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amewataka kutekeleza mikakati na maazimio ambayo wamekubaliana ili kila kata iweze kufika malengo katika shughuli za lishe
“Mikakati ambayo tumejiwekea katika kikao hiki mkayasimamie na kuyatekeleze ili tuweze kufikia malengo yetu katika suala la lishe,”amesema Mkurugenzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa