Na Kitengo cha Mawasiliano
Wataalamu kutoka Wizara ya Elimu na Chuo cha Ufundi Stadi VETA Makao Makuu wamefanya ziara ya kuja kuangalia eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Chuo cha Ufundi Stadi VETA katika Kata ya Kitama Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba na kuridhika na eneo hilo
Ziara hiyo imefanyika Disemba 12,2022 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani,Mwenyekiti wa Halmashauri,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na baadhi ya Wakuu waIdara na vitengo wamewaongoza wataalamu hao katika eneo ambalo limetengwakwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo
Wataalamu ambao wamefanya ziara ya kuangalia eneo la mradi ni Mbunifu Majengo Ndg. Dotto Saganda kutoka VETA Makao makuu na Mhandisi Samweli Bundala kutoka Wizara ya Elimu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa