Na Kitengo cha Mawasiliano
Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamehudhuria Mafunzo ya Mfumo wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao( National e-Peocurement System of Tanzania _NeST) Mkoani wa Mtwara
Akifungua mafunzo hayo leo Agosti 28,2023 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Nanjiva Nzunda amewasisitiza wataalamu hao kuhakikisha wanajifunza ili baada ya mafunzo hayo waweze kuutumia Mfumo huo
"Hakuna manunuzi yoyote yatakayofanyika nje ya Mfumo wa NeST , nategemea mkitoka hapa mtakuwa mabalozi wazuri kwa wengine,"amesema Nzunda.
Kwa Upande wake mmoja wa waratibu wa Mafunzo hayo Theresia Nsunzigwanko amezitaja Baadhi ya Faida za mfumo huo kuwa ni pamoja na kusajili taarifa mara moja na kuzitumia kwa zabuni zote zinazoombwa na hivyo kupunguza muda unaotumika katika kuomba zabuni
Amesema Mzabuni hatakuwa na haja ya kuweka viambatanisho vya vyeti au uthibitisho wa usajili kutoka kwenye Taasisi mbalimbali bali atatakiwa kuweka namba ya Uthibitisho .
Aidha Serikali inalenga kuwa ifikapo Oktoba 1, 2023 manunuzi yote yapitie Mfumo huo.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa