Na Kitengo cha Mawasiliano
Wasimamizi wa sensa ya watu na makazi 1284 wameanza mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Mafunzo hayo ya sensa ya watu na makazi 2022 yameanza Julai 31,2022 ambapo wamepangwa katika vituo vitatu ambavyo ni kituo cha mafunzo cha Tandahimba,Mahuta na Luagala
Katika Jumla ya wasimamizi 1284 Wasimamizi Maudhui idadi yao ni mia moja kumi na mbili (112) Tehama idadi yao thelathini na mbili (32) na Makarani idadi yao ni elfu moja mia moja na arobaini (1140)
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 Halmashauri ya Tandahimba Ndugu.Karim Mputa amewataka washiriki wote kuzingatia mafunzo hayo ili zoezi la sensa likamilike kwa asilimia mia moja
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa