Na Kitengo cha Mawasiliano
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tandahimba Ndg.Mussa Gama amewataka wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo ambao watasimamia uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Mndumbwe kuzingatia Sheria ,Kanuni na Maelekezo yanayotolewa ili kuwezesha zoezi la uchaguzi kufanyika katika hali ya Uhuru ,usawa na haki
Ameyasema hayo Disemba 14,2022 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wasimamizi wa vituo vya uchaguzi ambayo ynafanyika katika ukumbi wa mikutano ya Halmashauri
“Mmeaminiwa na kuteuliwa kwasababu mnao uwezo wa kufanya kazi hii ,hakikisheni mnazingatia maelekezo mtakayopewa badala ya kufanya kazi kwa mazoea”amesema Msimamizi wa Jimbo
Aidha Msimamizi wa Jimbo amewaapisha wasimamizi hao ili kufanya kazi hiyo kwa weledi kwa kuzingatia,taratibu,kanuni,miongozo na sheria ya Uchaguzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa