Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machella amewataka wasismamizi wa miradi kuisimamia na kuitunza miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao na wananchi washirikishwe katika miradi ili ikamilika iweze kukamilika kwa ubora na wakati muafaka
Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu mipya ya shule kupitia programu ya Lipa Kulingana na matokeo(EP4R) iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri
Wasimamizi wa miradi wa EP4R wakiwa kwenye mafunzo
Aidha amesema Mradi huo ambao ni zaidi ya Shilingi Bil 1 ni motisha kwa shule za msingi na sekondari kwa kwa ajili ya miundombinu ya Vyoo,madarasa na mabweni kwa ajili ya wanafunzi
“Mnatakiwa kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yenu ili wananchi wanufaike nayo lakini pia simamieni na kuitunza iwe katika viwango bora vinavyohitajika,”amesema Machella
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ally Machela (mwenye shati la maruni) ambaye alifungua mafunzo hayo
Naye Afisa Mipango wa Wilaya Hassan Nzyungu amesema kuwa miradi hiyo inahitaji kufuata taratibu ,kanuni na sheria kuanzia michoro,manunuzi,utoaji wa taarifa za utekelezaji kuanzia ngazi husika kwa muda muafaka
Afisa Mipango Hassan Nzyungu akielezea jambo kwa washiriki
Aidha naye Afisa Elimu Msingi Wilaya Hadija Mwinuka amesema kuwa pamoja na miradi hiyo kutekelezwa katika maeneo mbalimbali wananchi wanatakiwa kushiriki kwa kujitoa ili miradi hiyo iweze kumalizika kwa asilimia 100
Afisa Elimu Msingi Hadija Mwinuka akitoa ufafanuzi kwa washiriki
“Serikali inaongeza nguvu pale ambapo wananchi wameanzisha mradi katika maeneo kama ni shule,zahanati,soko na miradi mingine kwaiyo wananchi washirikishwe kwakuwa hii miradi ni yao,”amesema Mwinuka
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa