Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wasimamizi wa miradi wametakiwa kutumia utaratibu wa ’force account’ kwa kuzingatia sheria na kanuni ili kuweza kukamilisha utekelezaji wa miradi kwa wakati
Akizungumza kwenye kikao kazi cha wasimamizi wa miradi ngazi ya vijiji na kata Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Ally Machela amesema kuwa katika utekelezaji na ukamilishaji kanuni na sheria za fedha lazima zifuatwe
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Ally Machela akitoa neno kwa wasimamizi wa miradi
“Ni utaratibu wetu kukumbushana katika kutekeleza miradi kwenye maeneo yetu hivyo mna jukumu la kusimamia miradi iweze kukamilika kwa wakati na ubora kwa kufuata utaratibu wa kutumia force account,”amesema Ndg Machela
Wasimamizi wa miradi wakifuatilia mafunzo kutokakwa mwezeshaji (hayupo pichani)
Naye Ramadhani Mwita akiongea kwa niaba ya Afisa Mipango wa Wilaya amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwenye idara ya Elimu na Afya kwenda kukamilisha vyumba vya madarasa ,mahabara na kuweka vifaa muhimu sambamba na kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati
Ndugu Ramadhani Mwita akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa niaba ya Afisa Mipango Wilaya
Aidha naye Afisa manununzi faraji Kulodya alibainisha kuwa kamati zilizopo katika maeneo husika wahakikishe shughuli za manunuzi zinazingatiwa kwa kufuata taratibu,sheria na muongozo wa manununzi katika kutekeleza miradi hiyo
Mwezeshaji ndg . Faraji Kulodya akisistiza wasimamizi kufuatasheria ya manunuzi kwenye miradi
Katika mafunzo hayo wawezeshaji wameweza kuwasistiza wasimamizi na viongozi wa miradi kuweza kusimamia miradi hiyo ili iweze kuwa na tija kwa wananchi,fedha hizo zimetolewa na na Serikali kuu ,mpango wa kuendeleza Elimu ya msingi (PEDEP)Mpango wa maendeleo elimu sekondari (SEDEP) na WASH
Mwezeshaji wa mafunzo ndg Kassim Lihumbo akitoa mafunzo kwa washiriki
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa