Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wasimamizi na kamati wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia mipango kazi ya ujenzi wa miradi ili ikamilike kwa wakati
Akifunga kikao kazi cha wasimamizi na kamati za kusimamia miradi inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka kutekeleza jukumu hilo kwa weledi
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akisistiza jambo kwa wasimamizi na kamati ya miradi ya maendeleo(Hawapo pichani)
"Nawapongeza kwa kusimamia miradi lakini tuongeze usimamizi kwa kuweka maslahi ya Tandahimba yetu mbele ili miradi hii iweze kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia mipango kazi ya ujenzi wa miradi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amesema kuwa kikao kazi kitaongeza ufanisi wa kusimamia miradi hiyo iweze kutekelezwa kwa wakati na ubora unaohitajika kwa kukumbushana katika mada muhimu
“Tuna kila sababu ya kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jitihada inayofanya kuhakikisha inaboresha miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya kwa kuongeza vituo vya afya ambapo awali vituo vya afya vilikuwa vichache katika Halmashauri yetu jukumu kubwa ni kuisimamia ikamilike kwa wakati,”amesema Mkurugenzi
Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Mussa Gama (kati) akifungua kikao kazi cha wasimamizi na kamati za miradi ya maendeleo
Aidha ameeleza kwa muda mfupi Serikali imeongeza vituo vya afya vitatu katika Tarafa ya Litehu,Mihambwe,Mambamba ambapo awamu ya kwanza shilingi milioni 750 na tayari kiasi kingine cha shilingi milioni 750 kinaendelea kukamilisha miradi hiyo ambapo gharama ya miradi yote mitatu ya vituo vya afya ni shilingi Bil.1.5
Ongezeko la vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi, kwa sasa vituo vya afya vya serikali ambavyo vinaendelea kutoa huduma ni viwili (2) lakini miradi ambayo inaendelea na ipo katika hatua za ukamilishaji jumla ni vituo vinne(4) ambavyo ni Kituo cha afya Litehu,Mihambwe,Mambamba na Maheha ambavyo fedha zake zimetoka Serikali Kuu na mradi mmoja(1) wa kituo cha afya kitama ambao unaendelea kutekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 400 kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa