Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji na usimamizi wa miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa chini ya mpango wa kunusuru kaya maskini wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)wametakiwa kuibua miradi yenye tija na inayotekelezeka kwa wananchi wa maeneo husika
Mwezeshaji wa TASAF Amadeus Mbuta akitoa mafunzo kwa washiriki katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Hayo yamesemwa na Afisa Mazingira wa Tasaf Amadeus Mbuta wakati akitoa mafunzo kwa washiriki 45 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kusistiza kuwa miradi inategemea washiriki hao kuibua katika maeneo husika ambayo itawanufaisha jamii
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo
“Naamini baada ya mafunzo yanawapa uwezo wa kwenda kuibua miradi yenye tija na inayotekelezeka katika maeneo ambayo mtapangiwa ,”amesema ndugu Mbuta
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo
Naye Mratibu wa TASAF Tandahimba Ismaely Mbilinyi amesema mafunzo yaliyotolewa na wawezeshaji wa Kitaifa yameongeza ari kwa washiriki kuibua miradi inayotekelezeka katika maeneo husika kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya TASAF
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi akitoa neno kwa washiriki
Aidha wawezeshaji wa mafunzo hayo ya siku sita wamefundisha mada mbalimbali ambazo zimejenga uwezo kwa washiriki kuwa na uwezo wa kutekeleza jukumu la uibuaji wa miradi katika maeneo watakayopangiwa
Mwezeshaji Godius Johnas akitoa mafunzo kwa washiriki jinsi ya kuandaa mradi wa tengamaji
Naye mshiriki wa mafunzo Neema Shungu amesema kuwa mafunzo hayo yameongeza uelewa katika kutekeleza miradi ya TASAF na kuwaomba washiriki wengine kuzingatia ili yaweze kuleta manufaa kwa jamii na wananchi wa Tandahamba
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo ya utekelezaji na usimamizi wa ajira za miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa