Na Kitengo Habari na Mawasiliano
Washiriki 652 wamepewa mafunzo ya kuingiza taarifa kwenye mfumo katika operesheni ya anwani za makazi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Washiriki wa kuingiza taarifa kwenye mfumo wakipewa mafunzo
Akitoa mafunzo kwa washiriki katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Afisa Tehama Wilaya ya Tandahimba ndugu Joseph Mongi amesewataka vijana hao kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa umakini ili kuingiza taarifa sahihi
“Hakikisheni kuwa mtakapoanza kuingiza taarifa hizi muwe makini sana ili kuingiza taarifa sahihi ambazo zitatusaidia katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika Wilaya yetu,”amesema ndugu Mongi
Aidha amesema kuwa vijana hao wametoka katika vitongoji ambavyo wanaishi hivyo watakuwa na uelewa mzuri wa maeneo yao kwakuwa wanaishi kila siku
“Mmeaminiwa na viongozi wa vitongoji vyenu naamini mtapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa jamii mnazotoka mkaingize takwimu sahihi ambazo zitasaidia katika kitongoji ,kijiji,kata na Wilaya kwa Ujumla,”amesema ndugu Mongi
Mwezeshaji ndugu Zuberi Sarahani akifafanua jambo kwa washiriki
Washiriki hao wamepatikana kutoka katika kila kitongoji ambapo wataingiza taarifa za anwani za makazi katika vitongoji vyao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa