Na Kitengo cha Mawasiliano
Wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameshiriki kujaza kifusi katika ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa ambapo Serikali imetoa shilingi Mil,200 kwa ajili ya Utekelezaji wake ikiwa ni maandalizi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023
Zoezi la kujaza kifusi limefanyika leo Oktoba 21,2022 na wananchi wa Kata ya Malopokelo,Kwanyama na Mndumbwe ambapo ambapo Ujenzi wa miradi hiyo inatekelezwa
Wananchi kwa nyakati tofauti wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa madarasa hayo ambayo yatasaidia wanafunzi watakaochaguliwa wote kuendelea na kidato cha kwanza mwaka 2023
Fedha hizo zinatekeleza Ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa Shule ya Sekondari ya Tandahimba kwa gharama ya shilingi Mil.80,Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Sekondari ya Kwanyama kwa gharama ya shilingi Mil.60 na Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Sekondari ya Mndumbwe kwa gharama ya shilingi Mil.60
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa