Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Zoezi la Kampeni maalum ya utoaji wa Elimu na chanjo ya UVIKO -19Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba linaendelea vizuri ambapo wananchi wanaendelea kupata elimu na kuchukua hatua ya kuchanja kwa hiyari katika maeneo yao
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akizungumza na wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala katika ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na kusikiliza kero zao anatumia nafasi hiyo kutoa elimu ya chanjo ya UVIKO -19 kwa wananchi
Watoa huduma za afya wakiwa kwenye kikao kazi
Dc Sawala amesema ili wananchi wapate elimu hiyo anaambatana na watoa huduma ya afya ili kusogeza huduma kwa wananchi wa vijijini ambao baada ya kusikia elimu watakuwa tayari kupata huduma hiyo
Mtoa huduma ya afya akitoa elimu ya UVIKO -19 kwa mwananchi wa kijiji cha Dinyeke
“Katika ziara hizi ambazo nazifanya nimeona niwe naambatana na watoa huduma wa afya vijijini ili watoe elimu na chanjo kwa atakaye hitaji,kwa baadhi ya vijiji ambavyo nimefanya hivyo wananchi wamechanja kwa hiyari,”amesema Dc Sawala
Watoa huduma wa afya wakitoa elimu na chanjo ya UVIKO -19 katika viwanja vya shule ya msingi Amani kwenye bonanza lililoandaliwa na Benki ya NMB
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba inaendelea na kampeni ya utoaji Elimu na chanjo ya UVIKO - 19 ambayo imeanza rasmi tarehe 1/10 hadi 15/10 mwaka huu ambapo elimu hiyo inatolewa katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa