Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya sensa Wilaya Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa sensa ya majaribio ambayo inafanyika katika kijiji cha bandari kitongoji cha Ruvuma kata ya Michenjele inaendelea vizuri kwakuwa wananchi wametoa ushirikiano kwa makarani wanaochukua taarifa
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akieleza jambo
Ameyasema hayo katika kijiji cha bandari ambapo zoezi hilo la sensa ya watu linafanyika na kueleza kuwa sensa hiyo ya majaribio itatoa dira katika sensa ya mwaka 2022
Kamati ya sensa Wilaya ,Mkoa na wasimamizi wa sensa ngazi ya Taifa wakiwa kwenye picha ya pamoja
“Kamati ya sensa Wilaya na Mkoa tupo hapa kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia mia moja,makarani wamepita kaya hadi kaya na sasa wanaendelea na dodoso la majengo ambapo majengo yatahesabiwa , naendelea kuwasistiza wananchi kutoa taarifa sahihi kwa maendeleo ya nchi na Wilaya kwa ujumla,”amesema Dc Sawala
Naye Msimamizi wa sensa kanda ya kusini Ephraim Kwesigabo amesema zoezi hilo linafanyika kwa ushirikiano mkubwa wa Wilaya na Mkoa hivyo changamoto ambazo zitapatikana katika zoezi hilo la majaribio zitasaidia kuboresha mfumo wa sensa mwaka 2022
Msimamizi wa sensa kanda ya kusini Ephraim Kwesigabo akiwashukuru kamati kwa ushirikiano
Amesema sensa ya majaribio imeongeza madodoso ili kupata taarifa ambazo zitasaidia kujua kila kitu katika eneo husika ambapo kuna dodoso la kijamii,dodoso la hesabu ya watu ambalo lina maswali 97,dodoso la majengo na dodoso la anwani
baadhi ya majengo ambayo pia yatahesabiwa kwenye sensa ya majengo kijiji cha bandari
Nao wananchi wa kijiji cha bandari kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali kwa zoezi hilo ambalo litasaidia kuleta maendeleo katika maeneo husika,Mkoa wa Mtwara umekuwa miongoni mwa Mikoa 13 ambayo inafanya sensa ya majaribio ambapo Wilaya ya Tandahimba ni Wilaya pekee ndani ya Mkoa inafanya zoezi hilo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa