Na Kitengo cha Mawasiliano
Wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametoa maoni,kero mbalimbali na mapendekezo yao kuhusu maboresho ya mfumo wa Hakijinai kwa Tume ya Rais ya Hakijinai
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya shule ya msingi Amani Februari 27,2023 Profesa Edward Hoseah amesema kuwa kero ,maoni na mapendekezo ambayo wametoa yatawezesha Serikali kufanya maboresho katika vyombo vya mahakama,Jeshi la Polisi,Magereza,Taasisi ya Takukuru na Uhamiaji
Kwa upande wa wananchi walitoa maoni yao kuhusu Jeshi la Polisi kutumia busara pale inapobidi,ucheleweshaji wa kesi mahakamani,dhamana iwekwe bayana,mahabusu kutofika kwa wakati kusikiliza kesi zao,kujengwe gereza katika Wilaya ya Tandahimba
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewapongeza wananchi kuwa huru kutoa maoni na mapendekezo yao ambayo yataiwezesha Serikali kufikia malengo ya kuboresha mfumo wa hakijinai
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa