Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akipanda mche wa mti katika zoezi la upandaji miti kijiji cha Litehu
Na Kitengo cha Habari na Mawasilano
Wananchi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kupanda miti katika maeneo yao na kuitunza ili iweze kuwasaidia katika shughuli mbalimbali sambamba na kuhifadhi vyanzo vya maji
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba wakati akizindua zoezi la upandaji miche ya miti zaidi ya elfu 2000 katika kijiji cha Litehu jana
“ Mmejitokeza wengi katika zoezi hili nimefarijika sana kuwa mnaelewa umuhimu wa kupanda miti katika maeneo yanayotuzunguka kwakuwa miti inafaida nyingi ikiwa pamoja na kutunza vyanzo vya asili vya maji,’amesema Waryuba
Afisa Kilimo Horoun Kisimba akiwaelekeza wananchi jinsi ya upandaji wa miche hiyo
Naye Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka amesema kwa jinsi ambavyo wananchi wamejitokeza katika zoezi la upandaji wa miti ana Imani miti ambayo wataichukua na kwenda kuipanda katika maeneo wanayoishi wataitunza
“Kwa umoja huu ambao mmeuonyesha inadhihilisha wananchi wa Litehu hata miti hii ambayo mnapewa leo kwenda kuipanda na mtaitunza ili iweze kuwasaidia,”amesema Msomoka
Katika hatua nyingine Mhifadhi Misitu Wilaya ya Tandahimba Mohamed Mkubagwa ameeleza kuwa miti ambayo imepandwa na wananchi katika kijiji cha Litehu ni pamoja na Mitiki,albolea,mvule,msindano pamoja na miti ya matunda
Katibu Tawala Benaya Kapinga (katikati)akiwa tayari kwa kupanda mche wa mti
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa