Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wananchi wa Wilaya yaTandahimba wameipongeza serikali kuleta daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kwakuwa imewasaidia kuboresha taarifa zao na ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha wamefanikisha zoezi hilo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye vituo vya kujiandikishia wananchi hao wamesema wameridhishwa na zoezi hilo kwakuwa wamepata fursa ya kuwafuta ndugu na jamaa ambao wamefariki dunia na kuboresha taarifa zao
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kuboresha taarifa zao kwenye daftari ya kudumu
“Tunaishukuru Serikali kwa zoezi hili mimi nilikuwa Mkoa mwingine lakini kwa sasa nimehamia hapa nyumbani kwaiyo nimekuja kuboresha taarifa zangu kwa sasa nitapiga kura katika kata ya Ngunja,”amesema Twaha saidi
Mkazi wa Kata ya Ngunja akichukuliwa alama za Vidole na Bvr operator(kushoto) ni Maafisa Tehama wakiangalia zoezi linavyokwenda
Naye mkazi wa Mkwiti Kwenadi Masuka amesema pamoja na uwendeshaji wa zoezi hilo anaishukuru Wilaya imezingatia tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid – 19 katika vituo hivyo zoezi hilo kuendeshwa kwa amani
“Utaratibu ambao wameuweka ni mzuri wa kujikinga na ugonjwa huu wa korona kwakuwa watu ambao tumekuja kituoni tunaambiwa na mtu maalum ambaye anatusistiza kukaa mbali kati ya mtu na mtu pia kunawa mikono na maji tiririka na sabuni,”amesema Masuka
Mwananchi akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwenye kituo cha Kata ya Mkwiti kabla ya kupata huduma
Zoezi la uboreshaji awamu ya pili umekamilika ulianza Mei 02 na kumalizika Mei 04 mwaka huu kwa Kata zote za Tandahimba na wananchi wamejitokeza kupata huduma katika maeneo yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa