Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wananchi Wilaya ya Tandahimba wameipongeza Serikali kwa jitihada wanazozifanya kwa kutoa Elimu ya afya ya kujinga na magonjwa yanayoambukiza katika jamii hususan vijijini
Mwezeshaji akigawa na kubandika majarida yanayohamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameonekana kuridhishwa na mwenendo mzima wa serikali ya awamu ya tano kwa kutoa elimu ya afya kuanzia ngazi za vijiji na jinsi ilivyofanikiwa mapambano ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona(Covid -19)
Wakazi wa kijiji cha Maundo sokoni wakisikiliza matangazo kwa njia ya magari yanayohamasisha umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari
Bakari Said mkazi wa kijiji cha Namahonga Kata ya Maundo amesema kuwa ingawa ugonjwa huu hapa nchini umepungua lakini matangazo na majarida yanasaidia kukumbusha jamii kuendelea kuchukua tahadhari
Bashiru Likoti mkazi wa minjenjele akionesha bango ambalo lina maelekezo ya kuchukua tahadhari
“Tunampongeza Rais wetu wa awamu ya Tano kwa jinsi ambavyo ametuondolea hofu na jitihada alizozifanya ya kupambana na ugonjwa huu, elimu iendelee kutolewa ili wananchi waendelee kuchukua tahadhari kwa kugawa mabango na vipeperushi,”amesema Said
Mwezeshaji Kulwa Samiji akitoa elimu kwenye kijiwe cha kahawa Kitama stand
Zoezi la utoaji wa Elimu ya afya kwa jamii linaratibiwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,OR-TAMISEMI kwa ushirikiano na Redcross Tanzania ambapo Kata 30 na vijiji vyake Halmashauri ya Tandahimba vimefikiwa na kupata elimu kwa njia ya matangazo na majarida
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa